Yapokonywa uanachama CAF
Zanzibar si nchi! Yapokonywa uanachama CAF
Shirikisho la Soka Barani Afrika,CAF limeipokonya Zanzibar uanachama katika shirikisho hilo, kwa madai kuwa utaratibu stahiki haukufuatwa.
Kwa mujibu wa BBC, rais wa CAF, Ahmad amesema visiwa hivyo havikustahili kupewa uanachama kulingana na kanuni za CAF na tafsiri ya nchi kama inavyofafanuliwa na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.
” Walipewa uanachama bila kanuni zilizowazi kuzingatiwa. CAF haiwezi kuruhusu wanachama wawili kutoka nchi moja. ”
” Ufafanuzi wa nchi unatoka katika Umoja wa Afrika pamoja na Umoja wa Mataifa, ” amenukuliwa Ahmad.
Zanzibar ilipewa uanachama wa kudumu mwezi Machi mwaka huu katika mkutano uliofanyika jijini Addis Ababa.
0 comments:
Chapisha Maoni