Wakazi Temeke wameombwa kujitoa katika suala la usafi ili kujikinga dhidi ya magonjwa ya mlipuko na matatizo mbalimbali yanayotokana na uchafu.Pia wamewaomba wafanya Biashara kuwa na kawaida ya kufanya usafi kabla ya kufungua biashara zao na baada ya kufunga biashara zao na sio kufanya jumamosi tu ndio siku rasmi ya usafi.
Katika tukio hilo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mhe:Hashimu komba Katibu tawala wilaya ya Temeke,Akishilikiana na diwani wa viti maalum Mhe:Mariam Mtemvu wamewataka wafanya biashara kuweka bidhaa zao katika hali ya usafi na kuchangia tozo ya usafi kwa lengo la kutatua changamoto ya vifaa vya kufanyia usafi.
Mbali na usafi viongozi hao waligusia suala la uharifu katika mitaa na kuwaomba wananchi kushirikiana katika kufichua uharifu ili kudumisha amani na ustaarabu wa Watanzania.Mwisho waliwaomba vijana na akina Mama kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali kama kwa sasa serikali imetoa milioni 800 kwa ajili ya kuwasaidia vijana na akina Mama kujikwamua kiuchumi na kujiajiri katika sekta binafsi na kuleta maendeleo ndani ya Temeke na Taifa kwa ujumla
0 comments:
Chapisha Maoni