MALIASILI YADAIWA KUTAKA KUPORA ARDHI YA WAKULIMA WA CHANIKA KWA NGUVU,WENYEWE WAKULIMA WAMUOMBA RAIS MAGUFULI MSAADA WA KUPEWA ARDHI YAO

Mgogoro wa Wakulima wa eneo la chanika umezidi kukua huku wananchi wakija juu na kuongea na waandishi wa habari kuomba msaada wa Uongozi wa Juu hususan Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutoa tamko dhidi ya Mali asili kuacha eneo hilo ambalo wanainchi wanadai ni lao na wanalimiliki kwa Mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Mgogoro huo ambao una pande mbili na kila pande kulalamikia pande nyingine kuwa inatumia nguvu kutaka kumiliki eneo hilo na kwa upande wa Mali asili wanadai kua wananchi wamevamia eneo la Mali asili ambalo lilikua linaitwa mzimbwi na kuwaomba waache kulitumia eneo hilo.

Kwa upande wa wananchi wanasema toka mgogoro huo uanze kumeshaundwa kamati nyingi na kufanya mikutano mingi ili kutafuta suluhu la tatizo hilo na mwishowe walipata haki ya kumiliki ardhi hiyo kutoka kwa aliyekuwa waziri wa ardhi Mhe:Tibaijuka baada ya kujilizisha na utafiti uluofanywa na wataalamu.Viongozi hao wa mitaa kwa pamoja wamekiri kuwa na vielelezo vinavyoonyesha uhalali wa umiliki wa eneo hilo toka kwa aliyekuwa waziri wa ardhi Mhe:Tibaijuka.

Pia wameongeza kuwa kwa umoja wao viongozi wa mitaa wamemfuata Mhe waziri wa ardhi Lukuvi na kupewa jibu kuwa vielelezo vyote vimepelekwa kwa waziri Mkuu na sasa wasubiri majibu kutoka kwa waziri mkuu.

Sasa wanashtushwa na kauli ya Maliasili kuwa kuna kesi mahakamani na wameshindwa wanatakiwa watoke jambo ambalo hawalifahamu na hawajawahi kufungua kesi,Pili walikuwa wanasubiri jibu la waziri Mkuu ambalo mpaka sasa hajatoa tamko lolote.Hivyo wamemwomba Mheshimiwa Rais kusikia kilio chao na kuwasaidia kupata ardhi yao .

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List