Mhe Ridhiwani Kikwete ametoa vitendea kazi kwa watendaji ikiwemo na usafiri wa pikipiki kwa lengo la kuinua utendaji na kuwafikia wananchi kwa urahisi.Hili litachochoa utekelezaji wao wa shughuli za kila siku na kufikia malengo waliyojiwekea katika halmashauri.
Akiongea na Mwandishi wa blog amesema Katika mpango Mkakati wetu wa kusaidia watendaji ndani ya halmashauri yetu, Tumejipanga kuwawezesha vitendea kazi ili kazi zifanyike vizuri.
Tulianza kuwapa pikipiki maafisa Mifugo wetu wanne na baada ya kukusanya nguvu ya kutosha tumewapatia pikipiki watendaji hawa 10 ili kukamilisha idadi ya watumishi 14 katika halmashauri. awamu inayokuja ni kuwaangalia Watendaji Kata zote ili kuweza kuwafikia wananchi waliotuchagua na kusikiliza shida zeo na kuzitatua.
Mwisho wanufaikaji wa msaad huo wameshukuru kwa kupata vitendea kazi na kuhaidi kushirikiana kwa ukaribu kufanikisha shughuli za maendeleo.
0 comments:
Chapisha Maoni