Siku chache baada ya Rais dkt Magufuli kuivunja bodi ya chama kikuu cha ushirika cha kagera wadau wameunga mkono uwamuzi huo na kusema kuwa wakulima wa kahawa bukoba wamekuwa wakidhulumiwa haki zao za msingi katika ushirika huo kwa kukosa uwelewa.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama cha bukoba Ndugu:Felician Muhandiki ambapo wanajiandaa kwa mwakani kununua kahawa tani miatatu akiongea na waandishi wa habari jijini dar es salaam.
Muhandiki amesema kumekuwepo na tatizo la wakulima kutokuwa na uwelewa wa kutosha kuhusu vyama vya ushirika haki zao hali inayotajwa kuendelea kuwanyonya kipindi cha mauzo ya zao
la kahawa. na kuiomba serikali iwapatie elimu wakulima waweze kupata uwelewa wa kutosha kuhusu ushirika.
0 comments:
Chapisha Maoni