Wananchi waishio Kata ya Yombo Vituka wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam maeneo ya Ndola Pamoja na wakazi wa Maeneo ya Sigara Yombo Vituka wameomba Viongozi watakaopata nafasi na kuchaguliwa kuweka kipaumbele cha ujenzi wa Barabara ya Kilima cha Nyani sababu imekuwa kero kubwa sana.
Wananchi hao wamedai kipindi cha Mvua wanashindwa kupita sababu inajaa maji na tope pia inakatika na kuweka mashimo makubwa yaliyojaa maji na kusababisha wanafunzi kushindwa Kwenda shule kutokana na miundombinu kuwa mibovu.
Akina mama Wajawazito wakati mwingine hukumbana na kadhia ya kujifungua njiani hata kupoteza Watoto kwa kushindwa kufika Hospitali kwa wakati kutokana na eneo hilo.
Wakazi hao wamedaii kipindi cha Kampeni wagombea wamekuwa wakitoa ahadi zisizotekelezeka au zinazotekelezeka ila wanshindwa kuwa na ufuatiliaji mzuri.
Wananchi wa kata hiyo ya Vituka wameonesha Imani kubwa na Mgombea udiwani ndugu Mustapha Kashakala,Wameomba awe mtekelezaji wa ahadi zake na kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo hususan na suala la mikopo kwa vijana na akina mama.Ulinzi na usalama wa Kata ya Yombo Vituka.
Diwani mtarajiwa Kupitia chama cha Mapinduzi (ccm) amesema amsikia vilio vyao hivyo wamwamini na wamchague kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
Naye Mgombea Ubunge jimbo la temeke kupitia chama cha Mapinduzi ccm Ndugu Mariamu Kisangi amesema amewasikia kilio chao.Suala la barabara ya Kilima cha Nyani atalifanyia kazi tu baada ya kumchagua na kufika Bungeni sababu ana uzoefu na alikuwa Mbunge viti Maalumu miaka kumi na tano kupitia chama cha Mapinduzi.
Wagombea hao kupitia ccm kwa nafasi ya Udiwani na Ubunge wameomba kura kwa nafasi ya Urais wamchague Mama Samia Suluhu Hassan ili mafiga matatu yatimie na kurahisisha utekelezaji wa ahadi na ilani ya ccm.
Kampeni za uchaguzi zikiendelea kwa vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu huku kila chama kikivutia wananchi wawachague viongozi kupitia vyama vyao.
0 comments:
Chapisha Maoni