Ya Neymar, ni harusi na msiba Brazil


NI kama vile upo katikati ya harusi. Unashangilia hotuba ya kila mtu anayekwenda mbele kuzungumza na kuwatakia maharusi maisha mema ya siku za usoni.
Ghafla simu yako inaingia ujumbe wa simu kuwa mzazi wako mmoja amefariki. Ndicho kilichotokea Brazil baada ya kushinda pambano lao dhidi ya Colombia.
Nilikuwa natazama pambano hilo nje ya Uwanja wa Maracana na mashabiki wa Brazil baada ya kutoka uwanjani kushuhudia Ujerumani ikiichapa Ufaransa.
Mabao ya Thiago Silva na David Luiz yaliwafanya Wabrazili wapige sana kelele mitaani. Kulikuwa na ngoma za samba katika kila eneo la Rio de Janeiro.
Kwa utamaduni wao, ukiwa na pesa nzuri unalipa unafunga mtaa. Unakodi gari kubwa lenye muziki na kisha watu wanaanza kucheza, wakila na kunywa.
Pia ndivyo ilivyokuwa usiku wa kuamkia Jumamosi. Uzuri wa Brazil starehe haijalishi umri wala jinsi. Mnacheza ngoma halafu ghafla anakuja bibi na mwanaye wanaanza kucheza.
Maisha yaliendelea kuwa hivyo hivyo kwa muda mrefu wa usiku. Lakini ghafla zikaja taarifa kwamba maumivu ya Neymar yatamweka nje kwa kipindi chote cha fainali hizo.
Hapo ndipo ungejua kuwa Wabrazili wanapenda watu wao. Brazil yote ilikuwa kimya. Hakukuwa na raha kubwa sana kama ilivyokuwa kabla haijatangazwa kuwa Neymar atakaa nje ya uwanja hadi mwisho wa fainali hizo.
Kwa ilivyo Brazil, kama zilivyo baadhi ya nchi nyingine za Ulaya. Neymar alikuwa ametengenezwa kuwa staa wa fainali hizi. Ndio utamaduni ulivyo kwa wenzetu.
Lazima awepo mtu ambaye dunia itamtazama yeye zaidi kuliko mchezaji mwingine yoyote hasa michuano inapofanyika katika ardhi yenu. Hapa Brazil kila kitu ni Neymar, Neymar, Neymar, Neymar.
Ukienda katika vituo vya treni kuna picha za Neymar. Ukienda vyoo vya viwanjani kuna picha za Neymar. Ukienda mahotelini kuna picha za Neymar. Ukienda katika sehemu za muziki kuna picha za Neymar.
Haijalishi kama kuna wachezaji wengine wana uwezo mkubwa kuliko yeye, lakini Wabrazili pamoja na Fifa walishaamua kumfanya Neymar awe staa wa michuano kwa sababu mbalimbali ikiwemo sababu za kibiashara.

kutoka mwana sport
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List