DR SHEIN AKIWA UNGUJA KUOMBA KURA ZA WANAANCHI KUWA RAIS KWA AWAMU YA PILI ZANZIBAR



DK.Ally Mohamedi Shein Mgombea Urais Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi Ccm akiwa katika Kampeni za kujinadi kwa Wananchi wa Unguja na Kisiwa cha Pemba awataka wananchi hao wamchague kwa maraya Pili hili aweze kutekeleza kwa yale aliyofanya kipindi chake cha hawamu ya kwanza akiwa Rais wa Zanzibar.

Dk. Shein amesema kipindi cha hawamu yake ya kwanza ameweza kuweka nchi katika usawa wa Amani kutokana na machafuko yaliyokuwa yakijitokeza,siasa za chuki,pia ameweza kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwepo Elimu,Afya Kilimo,Umeme,Maji,na Miundombinu ya Barabara.

Dk Shein ameomba wamchague tena kwa hawamu ya pili amejipanga na Serikali yake kutoa Elimu bure toka shule ya Hawali hadi sekondari kutakuwa amna kuchangia gharama zozote za ,pia Wazee hawata changia gharama zozote za Matibabu,kwenye Kilimo amejipanga kuleta Mbengu bora,Mbolea na kuongeza Maafisa Ugani kila Kijiji na Vitongoji vyake,hata hivyo Serikali ya Zanzbar hinatambua Uchumi wa taifa inategemea Kilimo hivyo imefanikiwa kujenga barabara karibu na bonde la Mpunga ili kuwasaidia wananchi wakivuna wasafirishe mazao kwa urahisi mazao kutoka Shambani kupeleka Sokoni.

Dk. Shein amesema hivi sasa mabadiliko ni makubwa katika sekta ya Kilimo wameandaa mikakati wa kuendeleza Kilimo cha Umwagiliaji badala ya kutegemea mvua huku Vijana zaidi ya 1000 wakipatiwa elimu ya Shamba darasa,Serikali inafahamu muhimili mkuu wa uchumi ni kilimo hivyo Serikali inawajibu wa kuweka Sera kwaajili ya kutafuta Masoko ili wakulima waweze kubadilika hali za kuweka tija ya maendeleo,amesema kipindi cha Uongozi wake ameweza kuinua uchumi wa Wakulima wadogowadogo kwa kuchangia asilimia 75 na wakulima wenyewe asilimia 25 katika kuongeza tija ya bidhaa za Kilimo .

\Dk Shein akiwa katika Viwanja vya Bungi mkoa wa Kusini Unguja  akihitimisha mzunguko wa Kwanza wa Kampeni akiomba kura kwa wananchi ifikapo Oktobar 25 2015 aliwataka wasifanye makosa bali wamchague tena kuwa Rais wa Zanzibar na Tanzania Bara ikiwaniwa na Dk Jonh Pombe Magufuli sambamba na viongozi wengine wawakilishi ,Wabunge na Madiwani wote wa Ccm

Naibu katibu mkuu Ccm Zanzibar Vuai Ally Vuai amewataka wananchi waendelee kuwa na Imani na chama hicho kwa kuwa kimefanya nchi hizi kuwa na amani na upendo kwa wananchi kuishi kwa usalama
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List