Mgogoro wa Malipo wajenzi wa daraja la kigamboni walilia mapunjo yao wakiomba Serikali iwasaidie kupata haki zao Waliokuwa wafanyakazi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni 136 ambao walisimamishwa kazi na mwajiri wao Kampuni ya MBEC. CHINA baada ya kudai mapunjo ya mshahara wa muda wa miaka mitatu wamefikisha malalamiko yao hayo kwa Baraza la Usuluhishi wakisikiliza kwa umakini majadiliano yaliyokuwa yakiendelea katika ofisi za Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, kwenye kikao cha Baraza la Usuluhisho baadhi ya wafanyakazi hao wamesema wanachoomba kwa sasa ni stahiki zao Wafanyakazi hao wameiomba Serikali iwasikilize kwa kuwa wamefanya kazi ngumu ya kujenga daraja hilo tangu lilipoanza 2012 walipoahidiwa kulipwa Shilingi 12.500 kwa siku lakini baadaye malipo hayo yalikiukwa na wao kulipwa Shilingi 5.500 kwa siku, wafanya kazi hao wajenzi wa daraja la Kigamboni wameomba shauri hilo lipelekwe mbele yamefanyika makubaliano hayo baada ya kuona wameshindwa kufanyika makubaliano hapo
Baraza la Usuluhishi manispaa ya Temeke
WAFANYAKAZI WALIOKUWA MAFUNDI UJENZI DARAJA LA KIGAMBONI 136 WADAI MAPUNJO YA NYONGEZA YA MSHAHARA WAO
-
06:50
0 comments:
Chapisha Maoni