Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA wamewapa Leseni ya kutoa huduma ya Mawasiliano Kampuni ya AGANO SAFI itakayokuwa ikitoa huduma kwa Wananchi ya kufanya malipo ya fedha kwa njia ya Mtandao. Aidha Sekta ya Mawasiliano nchini imekuwa ikijiimarisha kwa kuongeza wigo mpana wa fursa mbalimbali za Mawasiliano kwa maendeleo ya taifa hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia. Dk Ally Simba Mkurugenzi Mkuu wa TCRA anasema huduma hii itakuwa ikiwasaidia Wananchi kutumia Malipo ya Kifedha na kuwawezesha kulipia huduma mbalimbali za Kijamii na Uchumi. Ayaloo ya Nangolo Mkurugenzi AganoSafi pamoja na Prof Cuthbert Mhulla Mwenyekiti wa Bodi Agano Saf wameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano kwa kuwapatia Leseni ya kutoa huduma kwa Wananchi na Wananchi wameahidi kutoa huduma hizo kwa uwadilifu kwa kiwango cha ubora
KISARAWE KUKATA KEKI YA BIRTHDAY YA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
-
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti akizungumza kwenye mkutano na
Waandishi wa Habari hawapo pichani kulia kwake ni Hakimu Mkazi Mkuu
Mfawidhi wa Maha...
Saa 12 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni