Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Maambukizi ya Ukimwi, Dkt Fatma Mrisho amesema tatizo la Ukimwi bado ni kubwa kwa Vijana hali inayochangiwa na kufanya ngono zembe. Dkt Fatma amesema katika ukuaji wa tatizo hilo, Vijana wa Kike ndiyo wanaongoza kwa Maambukizi hayo ikilinganishwa na wale wa Kiume. hayo ameyasema wakati wa kufunga Semina ya Vijana kuhusu Ukimwi pamoja na Maambukizi ya VVU. James Kajingwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana nchini amewataka Vijana wajiepushe na Utumiaji wa Ulevi wa kupitiliza unaweza kuchochea tabia ya kufanya ngono zembe na kupelekea Maambukizi ya UVV, pia amewataka Vijana kujitambua sambamba kuwa Mabalozi wa wengine kwa ajili ya kulinda vizazi vijayo kwa kutoa elimu ya mapambano dhidi ya Maambukizi ya VVU
NCAA YADHAMIRIA KUONGEZA IDADI YA WATALII WA NDANI
-
Na mwandishi wetu
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imedhamiria kufanya kampeni kubwa za
kuhamasisha utalii wa ndani kwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kue...
Saa 14 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni