Kampeni za Uchaguzi Kata Mwabwepande



Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe Geofrey Timoth amewataka Wananchi wawe na Maono ili waweze kupata Kiongozi mwenye hofu ya Mungu atakaye kuwa na Mapenzi mema ya kazi yake ili aweze kutekeleza ahadi zake atakazo ahidi.

Timoth amesema anafahamu kero za Mwabwepande.Barabara ni kero kubwa hivyo wakimchagua atatekeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara zote kolofi pia na ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Mwabwepande itakayokuwa mkombozi kwa akina mama,Watoto na Wazee.Walemavu atahakikisha wanapata huduma kwa wakati.

Akiendelea kujinadi amesema miradi mingine kama Maji,Elimu,Nishati ya Umeme na fedha zinazotolewa na Manispaa za asilimia kumi za kinamama na Vijana na asilimia tano za Walemavu atasimamia kuhakikisha zinafika kwa walengwa ifikapo October 29th 2025 wanamchagua kuwa mbunge Jimbo la Kawe pia amemuombea nafasi ya Urais Mama Samia Suluhu kuwa Mchapakazi ametekeleza miradi ya maendeleo.


Udiwani wa kata Mwabwepande wamchague Andrew Mashimba ni kijana mchapakazi Msomi na mtu anayeguswa na maisha ya Vijana atakuwa naye kwenye vikao vya baraza la Madiwani watakuwa wanashirikiana kutambua na kutatua kero za Mwabwepande.


Mgombea wa nafasi ya Udiwani Kata Mwabwepande jijini Dar es Salaam Andrew Mashimba amesema tatizo la ajira kwa vijana analifahamu na kukosa mikopo ya Serikali badala yake wanakopa Pikipiki kwa gharama kubwa za marejesho atalifanyia kazi ikiwa watamchagua nafasi ya udiwani wa kata hiyo.Wananchi wameombwa wachague viongozi wote watatu watoke chama cha Mapinduzi Ccm Urais Ubunge Udiwani na watashirikiana kuleta maendeleo mbalimbali kuanzia,Afya,Elimu na miundombinu ya barabara.


Taifa lipo katika kipindi cha kampeni ifikapo October 29 wajitokeze kupiga kura wachague kiongozi wanayemtaka.




Share on Google Plus

About SDM PRODUCTION MEDIA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List