Mwenyeki wa UWT taifa Marry Chatanda akizindua kampeni ya Uchaguzi ya 14 Temeke wilaya ya Temeke jijini Dar es saalam amewaomba Wananchi ifikapo okotobar 29 2025 wawachague viongozi wa chama cha Mapinduzi Urais Ubunge Udiwani ili waweze pata maendeleo watakapo chagua Mafiga matatu
Akiongea katika Mkutano wa Adhara Uwanja wa Mapumba Temeke amesema mama Samia ni Mchapa kazi pia ameweza kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwepo ujenzi wa Barabara Umeme Maji Shule Vituo vya Afya Masoko Madaraja na garimoshi (Treni) za Umeme mabasi ya Mwendo kasi ambapo hivi sasa kuna mradi wa Maji Kidunda mradi huo watanufaika mikoa miwili Pwani na Dar es salaam.
Mgombea Ubunge Jimbo la Temeke Mariamu Kisangi amesema wakimchagua ataibadilisha Temeke kuwa yenye kiwango atatekeleza miradi ya maendeleo Afya Elimu Miundombinu ya Barabara Umeme na Maji na kusimamia pesa za Mikopo isiyokuwa na Riba ya Manispaa kwa Vijana akina mama na Walemavu
Mgombea nafasi ya Udiwani kata Temeke 14 Marianu Mtemvu amesema akichaguliwa atasimamia vizuri fedha za mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Temeke na watapunguza gharama za matibabu Kwenda mbali na makazi yao
Kampeni zikiendelea za uchaguzi Chama Tawala Ccm na Vyana vya upizani kila mmoja akijinadi kwa sifa za kuwatekelezea maendelo ya wananchi ya taifa.
0 comments:
Chapisha Maoni