MALAWI UCHAGUZI




 Rais wa zamani wa Malawi Peter Mutharika anaongoza katika uchaguzi uliofanyika ambapo alikuwa akikabiliana kwa mara ya nne na rais wa sasa Lazarus Chakwera, kulingana na matokeo ya awali. Mutharika amepata asilimia 51 ya kura halali zilizopigwa katika mabaraza 9 kati ya 36 ya nchi hiyo, ikilinganishwa na karibu asilimia 39 za Chakwera kulingana na matokeo yaliyohesabiwa na shirika la habari la Reuters, kwa kuzingatia matokeo yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi nchini humo. Mgombea anapaswa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura halali ili kutangazwa mshindi wa moja kwa moja, vinginevyo kutakuwa na duru ya pili ya uchaguzi. Wachambuzi wa kisiasa walitabiri kuwa uchaguzi huo wa Septemba 16, ungeshuhudia mchuano mkali  kati ya Mutharika na Chakwera, wagombea urais wa vyama vikuu viwili katika bunge la taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Share on Google Plus

About SDM PRODUCTION MEDIA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List