SHEIKHE MKUU WA DAR ES SALAAM AHIMIZA KUHIFADHI KITABU KITUKUFU CHA QURAANSHEKHE  mkuu wa Mkoa Dar es salaam Alhad  Mussa Salum  amewataka  Waislamu kote nchini kukihifadhi  Kitabu Kitukufu cha Quraan hatua itakayowapa Swawabu kwa Mwenyezi Mungu.

Ameyasema hayo hivi karibuni  katika viwanja vya Mwembe yanga jijini Dar es Salaam wakati akizindua Tamasha la maonyesho ya miujiza ya Kitabu cha quraan kilicho hifadhiwa kwa kipindi cha miaka 51.

Naye Hashimu Ramadhani amewataka waislamu kuachana na mambo ya kidunia badala yake wafuate dini ya kiislamu inavyotaka kumcha na kumtumikia mwenyezi mungu ili waweze kupata swawabu na masuala yao yatakuwa ya kheri na yenye Baraka.

Osama Ismail ambaye alikuwa mshiriki katika tamasha hilo aliweza kuonesha kipaji  chake cha uwezo mkubwa wa kusoma kitabu Quran.

Mbali na hayo kijana Mohamed Tagy Khany amewataka waislamu kuhifadhi Quran kwa miaka 51 kwa kuwa ni vema waislamu kuchukua mafunzo yote ya kitabu hicho an kufuata sheria za mungu.
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List