WAKULIMA PWANI WAHIMIZWA KUBORESHA KILIMO

             

 

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza amesema Mkoa huo umejipanga kuboresha kilimo kwa kila kaya kulima heka tatu kwa ajili ya chakula na biashara ili iweze kujiinua kiuchumi na kuondokana na utegemezi usio na ulazima.
Mahiza aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kuwa pamoja na mkakati huo wananachi wa mkoa huo wanatakiwa kuweka akiba ya vyakula.
“Tusikubali kutaabika kwa umasikini na njaa hivyo ni vema kila kaya kulima mazao ya aina tatu,  likiwemo zao la biashara, zao la chakula pamoja na mazao mengine kwa ajili ya kujiwekea akiba,” alisema Mahiza

Pia mkuu wa moa huyo aliahidi kufanya ziara na maafisa ugani pamoja na wataalamu wa masuala ya kilimo ili kutoa elimu ya kilimo bora na uwajibikaji kwa wakulima.
Naye Mkurugenzi wa Kibaha vijijini, Tatu Mwantumu aliunga mkono jitihada hizo za Serikali na kuwataka wananchi kuitumia ipasavyo ardhi ya mkoa huo kwa kuwa ina rutuba safi.
Aliwataka wakulima kulima  zao la ufuta, mihogo, alizeti na korosho kwa kuwa mazao hayo yanaweza kuwanufaisha.

Pia aliwataka kuacha kuchoma moto mashamba ya mikorosho na miembe kwa kuwa wanaisababishia  ardhi kukosa rutuba.

 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List