WAVUVI WA SAMAKI WILAYA YA BAGAMOYO WALIA NA UKOSEFU WA VIFAA DUNI VYA UVUVI


Na Gloria Matola

WAVUVI wa Samaki Wilaya ya Bagamoyo wako katika wakati mgumu wa kimaisha kutokana na ukosefu wa vifaa vya  uvuvi.

Kutokana na hali hiyo wakazi wengi wa eneo hilo wamejikita katika uvuvi haramu ili kujiinua kimaisha na kupata kitoweo.

 

 

 

Wavuvi hao wakizungumza na waandishi wa habari, pembezoni mwa fukwe ya bahari ya Hindi eneo la Bagamoyo walisema kuwa wanatambua kuwa uvuvi haramu siyo mzuri kutokana na ukweli kuwa unaua mazalio ya Samaki na kuathiri mikoko.

Mmoja wa Wavuvi hao, Shaban Kassim alisema kuwa hawapendi kuvua kwa baruti wala nyavu haramu pamoja na vifaa vinavyoharibu mazalia ya samaki na mikondo ya Bahari lakini inatokana na hali duni.
Mvuvi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Ramdhani Swalehe ameiomba serikali kuwa makini na fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa jamii na kuhakikisha inawafikia walengwa.

Alisema Serikali imekuwa ikijitahidi kutoa pesa kupitia kwenye halmashauri za wilaya nchini lakini utekelezaji wa miradi hiyo imekuwa ni changamoto kwa jamii nchini wakiendelea kuishi maisha ya kimasikini chini ya dora moja kwa kaya.

Serikali pamoja na jitihada za kutokomeza umasikini lakini bado mafanikio kwa wananchi inatakiwa kuendelea jitihada za makusudi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kukuza uchumi wananchi.
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List