Na Gloria Matola
JAMII ya Watanzania
nchini imeshauriwa kuthamini na kununua bidhaa zinazotengenezwa nchini
ili kukuza soko la ndani pamoja na kuongeza
ajira kwa vijana ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.
Hayo yameelezwa na mjasiriamali wa Bagamoyo Wine,Teddy Alban
Davis ambaye ni mwekezaji mdogo wa mkoa wa Pwani wilaya ya Bagamoyo.
Teddy alisema changamoto kubwa
anayokabiliwa nayo katika uwekezaji mdogo ni ukosefu wa uwakika wa masoko ndani na nje kwa kuwa Watanzania hupenda
kununua bidhaa za kutoka nje wakidhani ndio bora zaidi.
Tedy alisema inatakiwa kuwe na ushirikiano kati ya Serikali
na Wajasiriamali wa ndani ili kazi zao ziwez kuthaminika na kupata nafasi ya
kuwepo katika maonyesho ya ndani, sabasaba, nanenane na kwenye maonyesho la
soko la afrika mashariki bila kubaguliwa.
Pia alisema katika mwezi mtukufu wa Ramadhani biashara
imekuwa ngumu kutokana na mkoa wa Pwani hususani wilaya ya agamoyo kuwa na waumini
wengi wa dini ya kiislam ambao wengi wao ufunga ili kukamilisha moja ya nguzo
tano za uislam.
Naye Imamu mkuu wa
Msjidi Ramiya, Maalim Simba Abuuqhari Ramiya amewataka Waislam wote nchini kuheshimu mwezi wa Ramadhani nakumtumikia mwenyezi Mungu kwa kufuata mambo
mema aliyoyafanya Mtume Mohamedi SW ili kushiriki ibada pamoja na kufunga kwa
ajili ya matendo mema ya Swawabu.
Maalim Simba alizungumza hayo kwa niaba ya mkuu wa Bagamoyo,
Sheikh Abdulqri Ramiya ambapo aliwataka wananchi wa wilaya hiyo na duniani kwa
ujumla kwa dini zao kuheshimiana na kupendana ili kuhepukana na migogoro isiyo
ya lazima.
Meya wa Bagamoyo ambaye pia ni mwenyekiti wa mji mdogo, Abdul
Zohoro Sharifu alisema mwezi huu ni vizuri waumini wakatoa msaada kwa jamii
isiyokuwa na uwezo ili kuwasaidia kupatafutari, kwa kuwa nao wanahitaji funga ya Ramadhani.
Meya huyo alisema yeye binafsi anafata njia za Mtume Mhamedi
SW njia zote za Imani ya Kislam,ameanza kutoa vyakula kwa kaya isiyo kuwa na
uwezo kimaisha kwa kata 22 kwa jimbo la Bagamoyo,Pia amegawa vitabu vya Quruani takatifu,Juzuu,Tasibini,Kanzu na
Kofia.
Sharifu alisema watanzania waachane na mtazamo mdogo kwa
baadhi ya wanasiasa kuwa wanapowasaidia wananchi wasiojiweza au kitu chochote
cha maendeleo kuwa unaitaji uongozi mtazamo huo unarudisha nyuma maendeleo ya
taifa.
0 comments:
Chapisha Maoni