

………………..
Na Concilia Niyibitanga- WHVUM
Serikali
kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imempongeza Mzee
Muhidini Gurumo kwa mchango wake uliotukuka katika tasnia ya Muziki
nchini pamoja na kumpongeza kwa kustaafu kazi hiyo.
Akiwasilisha
barua ya Serikali ya kutambua mchango wa nguli huyo juzi nyumbani kwake
Makuburi Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi.
Lilly Beleko amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wake
katika muziki wa Dansi hapa nchini.
‘Serikali
inathamini mchango wako katika Muziki hapa nchini na itaendelea
kuzienzi kazi hizo na inakupongeza kwa kazi nzuri ulioifanya ya
kuelimisha, kuhamasisha na kuburudisha jamii’. Amesema Bibi. Beleko.
Naye
Rais wa Shirikisho la Muziki nchini, Bw. Addo Mwasongwe, amesema kuwa
Shirikisho linampongeza kwa kazi zake nzuri na litaendelea kumtumia
katika kazi za muziki ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri katika tasnia
hiyo.
Nguli
huyo wa muziki wa dansi nchini katika enzi zake za uimbaji ametunga
nyimbo za kuelimisha jamii kufanya kazi kwa bidii, kudumisha usawa,
amani na kuwakumbusha wazazi kutimiza wajibu wao wa kuwalea watoto
katika maadili mema.
Mzee
Gurumo ambaye ameanza kazi ya muziki mnamo miaka ya 1960 na kustaafu
kazi hiyo mwaka huu amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa kutambua kazi
yake na amefarijika kwa kukabidhiwa barua ya kumtambua na kumpongeza kwa
kustaafu kazi hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni