Kaimu mwenyekiti mchungaji Sauli Kajula wa kanisa la Moravian jimbo la Misheni Mashariki na Zanzibar Temeke Dar Es salaam akiwaongoza waumini katika sara iliyofanyika kanisani hapo.
Waumini wa Kanisa la Moravian jimbo la Misheni Mashariki na Zanzibar Dar Es Salaam wakiwa katika misa.
Mchungaji akiwa na waumini wa kanisa la Misheni Mashariki la Moravian wakiwa katika misa wiki hii.
Waumini wakifuatilia sara kutoka kwa kaimu mwenyekiti Saul Kajula wa Jimbo la Misheni Mashariki na Zanzibar Dar Es Salaam.
Waumini wakifuatilia tamko lililotolewa na wawakilishi wa waumini juu ya mgogoro unaoendelea katika jimbo hilo la Misheni Mashariki na Zanzibar Dar Es Salaam.
Waumini wakifuatilia kwa makini wakati tamko linatolewa.
Waumini wakifuatilia hatua kwa hatua namna mgogoro huo utakavyotatuliwa na namna jinsi ulivyoaanza, ili watambue kifanyikacho lazima kiwe na tamati ili neno la Mungu litimizwe kwa busara.
Mchungaji Clementino Fumbo Hatakiwi kuongoza kanisa la Moravian Jimbo la Misheni Mashariki na Zanzibar kutokana na ubadhirifu wa fedha na yeye kusababisha mgogoro katika kanisa hilo pamoja na mtunza hazina Mrs. Nyambilila Lwago.
MSIMAMO WA WAKRISTO WATIIFU KWA KANISA.
Wakristo tunauomba umoja wa kanisa la Moraviani Duniani kusitisha kikao cha tamati inayotajwa kuwa ya mpito kwani kwa sasa kuna jitihada za kumaliza mgogoro zinazofanywa na Askofu Dr. L. Mwakifwila akishirikiana na Askofu A. Cheyo. Kuendelea na kikao hicho ni kutaharibu ratiba ya baba Askofu ambayo ipo kwa mujibu wa katiba ya kanisa kifungu na. 21. Wakristo hatutopenda kuona kikundi cha watu wachache kinavunja katiba ya kanisa iliyosajiriwa kihalali na mamlaka za serikali ili kukidhi mahitaji yao kwa nia mbaya ya kusababisha uvunjifu wa amani ndani ya kanisa letu la Moravian.
Waumini waniomba serikali kufanya mawasiliano yake na Jimbo kupitia Askofu Mwakafwila mlezi wa Jimbo ambaye pia ndiye mwenye jukumu la usuhulishi kwa sasa katika Jimbo.
Waumini tunamuomba sana, tena sana mchungaji Nosigwe Buya kuvaa uwakilishi stahiki wa umoja wa kanisa la Moravian Duniani bila kuegemea upande wowote.
Mgogoro huu umedumu kwa muda mrefu sana kwa sababu ya kundi lililokiuka taratibu za kanisa kuendelea kupata nguvu kutoka sehemu mbalimbali. Tunaomba taratibu za kanisa ziendelee kuheshimiwa na kulindwa. Tamko na msimamo huu umetolewa kwa pamoja na wakristo wa kanisa la Moravian Jimbo la Misheni Mashariki na Zanzibar ambao ni watiifu kwa kanisa na wanafuata taratibu za kanisa kama iliovyosajiriwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Nakala kwa;
- Ofisi ya Waziri mkuu
- Wizara ya mambo ya ndani
- Umoja wa kanisa la Moravian Duniani
- Maaskofu wote wa KMT
- Wenyeviti wote wa KMT
- Halmashauri kuu KMT - JMM
Mwanakondoo Ameshinda.........Tumfuate........!!!!!!!
0 comments:
Chapisha Maoni