Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara( wa
pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya Gari
la kurushia matangazo la TBC, kutoka kulia ni Makamu Waziri wa Biashara wa
Jamhuri ya watu wa China Li Jingzao, Makamu wa Rais wa China Li Yunchao na wa mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw.
Clement Mshana
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara akikabidhiwa mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia matangazo
la TBC mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa
Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Li Jingzao.
Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
akimkabidhi zawadi ya Kinyago cha mnyama Twiga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Watu wa China Li Yunchao mara baada ya kuzindua gari la kurushia matangazo la
TBC leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana
Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa
moja lililokabidhiwa kwa TBC likiwa katika viwanja vya Shirika hilo Mikocheni
jijini Dar es Salaam.

Kutoka kushoto ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba
Nkinga, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utawala Bora Kapteni George Mkuchika na
Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Clement Mshana wakifuatilia mazungumzo baina ya
Makumu wa Rais wa China Li Yunchao na Mwakilishi wa Startime (hawapo pichani)
alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Blogger Comment