WATU 15 MBARONI KWA KUTAKA KUMTOROSHA ASKOFU GWAJIMA

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia wafuasi 15 wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa tuhuma za kutaka kumtorosha Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Josephat Gwajima ambaye amelazwa katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni Dar es Salaam, baada ya kupata mshituko wakati akihojiwa na makachero wa Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, ilisema usiku wa kumkia jana, mmoja wa walinzi wa Hospitali ya TMJ alibaini njama za kutaka kutoroshwa kwa Askofu Gwajima ambapo alitoa taarifa polisi.
“Kutokana na hali hii, makachero wa polisi walifika eneo hilo na kukuta kweli kuna hali ambayo si ya kawaida kwa kuwapo kundi la watu. Wamekamatwa watu 15 na mmoja wao Ekomia Diagare, alikutwa na begi ambalo lilikuwa na vitu mbalimbali ambavyo alidai anampelekea Askofu Gwajima.
“Bastola aina ya Bereta yenye namba CAT 5802 ikiwa na risasi 3, risasi 17 za Shortgun, vitabu, hundi za benki, hati ya kusafiria yenye jina Gwajima Mathias Joseph yenye namba AB54480,” alisema Kamanda Kova.
Mbali na hilo, pia inadaiwa watu hao walikutwa na kitabu cha Benki ya Equity na hundi, nyaraka mbalimbali za Kampuni ya Puma, chaja za simu na suruali mbili, makoti mawili, fulana za ndani moja,soksi jozi mbili na nguo ya ndani.
Kamishna Kova, aliwataja watuhumiwa weingine kuwa ni Chitama Mwakibambo (32) , Edwini Audex (24), Adamu Mwaselele(29), Frederick Fusi (25), Frank Minja(24), Emmanuel Ngwela (28).
Wengine ni Geofrey William (30), Mchungaji Mathew Nyangusi (62), Mchungaji Boniface Nyakyoma (30), Geofrey Andrew (31), Mchungaji David Mgongolo (24), George Msava (45), Nicholaus Patrick (60) na Mchungaji George Kiwia(37).
'WATU 15 MBARONI KWA KUTAKA KUMTOROSHA ASKOFU GWAJIMA 

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia wafuasi 15 wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa tuhuma za kutaka kumtorosha Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Josephat Gwajima ambaye amelazwa katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni Dar es Salaam, baada ya kupata mshituko wakati akihojiwa na makachero wa Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, ilisema usiku wa kumkia jana, mmoja wa walinzi wa Hospitali ya TMJ alibaini njama za kutaka kutoroshwa kwa Askofu Gwajima ambapo alitoa taarifa polisi.

“Kutokana na hali hii, makachero wa polisi walifika eneo hilo na kukuta kweli kuna hali ambayo si ya kawaida kwa kuwapo kundi la watu. Wamekamatwa watu 15 na mmoja wao Ekomia Diagare, alikutwa na begi ambalo lilikuwa na vitu mbalimbali ambavyo alidai anampelekea Askofu Gwajima.

“Bastola aina ya Bereta yenye namba CAT 5802 ikiwa na risasi 3, risasi 17 za Shortgun, vitabu, hundi za benki, hati ya kusafiria yenye jina Gwajima Mathias Joseph yenye namba AB54480,” alisema Kamanda Kova.

Mbali na hilo, pia inadaiwa watu hao walikutwa na kitabu cha Benki ya Equity na hundi, nyaraka mbalimbali za Kampuni ya Puma, chaja za simu na suruali mbili, makoti mawili, fulana za ndani moja,soksi jozi mbili na nguo ya ndani.

Kamishna Kova, aliwataja watuhumiwa weingine kuwa ni Chitama Mwakibambo (32) , Edwini Audex (24), Adamu Mwaselele(29), Frederick Fusi (25), Frank Minja(24), Emmanuel Ngwela (28).

Wengine ni Geofrey William (30), Mchungaji Mathew Nyangusi (62), Mchungaji Boniface Nyakyoma (30), Geofrey Andrew (31), Mchungaji David Mgongolo (24), George Msava (45), Nicholaus Patrick (60) na Mchungaji George Kiwia(37).'
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List