Wafanyabiashara wa mboga mboga soko la ilala walalamikia miundombinu ya soko mibovu na chakavu

Wafanya biashara  wa soko  la ilala wauza mbogamboga wamesema wananyanyasika kwa kukosa eneo rasmi la kufanyia biashara pamoja na ushuru wanalipa kwa wakati.

Wakiongea na startv wameilalamikia miundombinu ya soko hilo sio salama ni chakavu na mibovu hali inayochangia kufulika kwa chemba za MAJI machafu na kuzagaa maeneo chini waliyopanga bidhaa zao.

Mwenyekiti wa wauza mbogamboga Ilala,Elita Rashid ameiomba Serikali kusikia kilio chao kwakuwa wanakabiliwa na hali ngumu kutokana na kukosekana kwa eneo rasmi la biashara.

Soko la ilala limekuwa na ongezeko kubwa la wafanyabiashara kutoka 2000 na sasa jumla yao in zaidi ya 5000 huku baadhi yao wakipanga bidhaa zao chini baada ya kukosa meza ya biashara.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List