Serikali imeombwa kuwa na huruma kwa wakazi waliobomolewa na
ambao wameendelea kuishi katika maeneo hayo ya mabondeni kwa kile kilichodaiwa
kuwa ni baada ya kukosa maeneo ya kwenda kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa.
Pamoja na madai ya serikali kuwa iliwapatia viwanja maeneo ya Mabwepande ,Wakazi hao wa Bonde la Mkwajuni Ananasifu wanakanusha kupewa viwanja hivyo kutokana na serikali iliandikisha wapewa viwanja 375 lakini waliopatiwa Viwanja ni nyumba 25.
Habiba Mondoma,Katibu wa Muunganowa serikali za mitaa 18 katika bonde la Msimbazi ameiomba serikali eneo la kwenda kutokana na wengi wao kutokuwa na uwezo wa kupata eneo la kuishi.
Baadhi ya wananchi waliokuwa wakiendelea kuishi eneo la Bondeni baada ya kubomolewa nyumba zao wameitupia lawama Serikali kuwa ilitakiwa wafike na kuonana na walengwa ili wajue kama kweli hivyo viwanja walipewa au imekuwaje wananchi hao wamekuwa wakiendelea kuishi hapo.
Mhandisi Bonaventure Baya,Mkurugenzi Mkuu NEMC amewaomba wananchi hao kukubaliana na agizo lililotolewa na serikali badala ya kuleta upinzani na kuheshimu sharia.

0 comments:
Chapisha Maoni