SERIKALI IMEWATAKA WAZAZI WAANDIKISHE WATOTO SHULE ILI KUWAPA HAKI YAO YA MSINGI
-Serikali imewaagiza wazazi na walezi wote nchini kuwapeleka shule watoto wote wenye umri wa kuanza elimu ya awali na msingi kwa mwaka huu wa 2016 ambapo Elimu inaanza kutolewa bure toka elimu ya awali hadi kidato cha nne kwa shule za serikali.
Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na watoto Ummy Mwalimu amesema ifikapo march 30,2016 Serikali kupitia mwanasheria mkuu itawafungulia mashitaka na kuwapeleka mahakamani wazazi na walezi wote watakao kuwa wameshindwa kuwapeleka watoto wenye sifa kuanza masomo.
Wakati huohuo amesema serikali imejipanga kuwaondoa barabarani watoto wote wanaotumikishwa na wazazi wao kuombaomba.Baadhi ya Madereva wanabainisha usumbufu wanaokutana nao kwa watoto hao ombaomba.
Rais wa awamu ya Tano Dr John Magufuri alifuta ada kuanzia elimu ya awali mpaka kidato cha nne ili kuhakikisha watoto wote wanakwenda shule na kupata elimu kwa kuwa ni haki yao kwa Mujibu wa sharia ya watoto namba 2 ya mwaka 2009.
0 comments:
Chapisha Maoni