Ofisi ya taifa ya takwimu imetoa tathimini ya mfumuko wa bei kwa mwaka uliopita 2015 ambao umepungua kwa asilimia 5.6 kutoka asilimia 6.1 kama ilivyokuwa mwaka 2014.Mkurugenzi wa sensa ya watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigambo amesema kupungua kwa mfumuko wa bei katika kipindi cha mwaka jana kulichangiwa na kushuka kwa kasi ya kupanda kwa bei zisizo za vyakula.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa sense ya watu na Takwimu za jamii ndugu Ephraim Kwesigambo amesema mfumuko wa bei zisizo za chakula ulipungua mpaka asilimia 1.8 kwa mwaka 2015 kutoka asilimia 4.9 ya mwaka 2014.Amefafanua mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwezi ambao umeongezeka kwa asilimia 0.5 ukilinganisha na ongezeko la asilimia 0.8 mwezi November 2015.
Amesema mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi za afrika Mashariki,ambapo kwa Kenya umeongezeka kwa asilimia 8.01 kutoka asilimia 7.32 kwa mwaka 2015 na Uganda umeongezeka hadi asilimia 9.30 kutoka asilimia 9.18.
0 comments:
Chapisha Maoni