KIJANA MDOGO ALIYEJITOKEZA KUWANIA NAFASI YA UBUNGE ATOA MAONI KWA UONGOZI MPYA WA RAISI WA AWAMU YA TANO MH: MAGUFULI


Kijana mkazi wa dar es salaam ambaye pia alikuwa ni mmoja kati ya watu waliotia nia na kugombea ubunge kupitia CCM kura za maoni  Jimbo la mbagala Bwana STUART GEORGE MATOLA ametoa ushauri kwa Mh:Magufuli na Baraza lake la mawaziri.Akiongea na mwandishi wa blog hii amesema;

Vitu anavyofanya Rais Magufuli ndivyo Watanzania wengi walitamani maraisi wa hawamu zilizopita wafanye,Hivyo nampongeza sana kwa kujitolea kutumbua majibu yeye binafsi na kuonyesha mfano mzuri sio kwa Tanzania tu bali Afrika na Dunia nzima.
Rais anatakiwa awe mfano wa kuigwa na kwa kipindi kifupi ametuonyesha hilo lakini ni mapema sana kusema moja kwa moja kuwa atafanya makubwa inabidi tumpe siku ili tutathimini ni kwa kiasi gani atakuwa ameweza kutekeleza Irani ya Chama cha mapinduzi na ahadi zote alizowahidi Watanzania.
Pia hakusita kusema kwamba kwa kiasi kidogo sana amefurahishwa na utendaji wa mawaziri na viongozi mbalimbali wa serikali kwa kuwa wamejikuta wakifanya mambo mengi kwa kufanya ili waonekane wanaendana na kasi ya HAPA KAZI TU wakati mambo ambayo wanatumia mda mwingi kufanya na hatua wanzochua si za msingi au Busara ya kutosha.Inabidi watulie kwanza waweke mipango na mashariti ya wizara zao na kuanza kusimamia utekelezaji wake kwa umakini zaidi.
"kwa maoni yangu ni bora mawaziri wateule wangekaa na kupanga mipango huku wakipitia mambo yaliyokwamisha wizara hizo kufikia malengo yake na sio kujipa kazi za Ulinzi au kuonyesha ukali tu wakati inawezekana hiko ni chanzo cha mwisho katika kutofikia malengo.Tunajua wizara ina watu wengi ambao wanaweza kufanya kazi hizo na kutumiza majukumu yao kama tu Waziri atakuwa na malengo thabiti na usimamizi wa utekelezaji wake"
Kijana huyo alimalizia kwa kusema Nawapongeza sana wote mliopata nafasi ya kuaminiwa na kufanya kazi na serikali yenye kasi kubwa ya awamu ya Tano.Nimalize kwa kusema Hapa kazi tu.


                                        
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List