UJENZI WA SHULE MAJIMATITU

Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi(UWT)wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam wametoa kiwanja chenye ukubwa wa ekari mbili na nusu kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi pamoja na vifaa vya ujenzi.
Pamoja na haya pia wamechangia matofali 1000 na mifuko ya saruji 752 na ahadi ya mifuko 200 sambamba na fedha laki tano za kuanzia ujenzi huo wa shule mpya ya Majimatitu Mbagala.Uamuzi huo umekuja kufuatia idadi kubwa ya wanafunzi katika shule za msingi kutokana na agizo la Rais  Dkt John Pombe Magufuli kuamuru kutolewa kwa elimu ya shule ya msingi na sekondari bure.
MAHESHI BORISHA ambaye alikuwa mgombea wa ubunge jimbo la mbagala kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi amesisitiza kuwa jamii iliyo elimika huchochea maendeleo kwa kasi zaidi hivyo ujenzi wa shule na utoaji wa elimu ni kitu cha msingi kwa taifa lolote linaloendelea,Pia ameomba wafanya biashara,wanasiasa na wadau wengine kujitokeza kuchangia utoaji wa elimu kwa sababu suala la elimu halina Chama.Maheshi Borisha kwa kuonyesha mfano amehaidi mifuko 100.
Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa amepongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wa kuagiza elimu ya Shule za msingi na sekondari itolewe bure.
Wengine waliokuwapo na kutoa ahadi ni Issa Ali Mangungu mbunge wa Mbagala ambaye alihaidi mifuko 2.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List