Wadau wa Michezo Nchini wameadhimisha miaka 52 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya mazoezi ya Viungo vya Mwili. Mazoezi hayo yameandaliwa na Manispaa ya Temeke kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Michezo kutoka Manispaa hiyo na,wamezialika timu mbalimbali ikiwemo Namanga Jogging Club ya Kinondoni. Mussa Mtulia ni Mwenyekiti wa timu Smart Member ya Temeke anasema wakiwa wadau wa Michezo nchini wameamua siku ya Muungano kusherekea kwa kufanya mazoezi. Watanzania katika maeneo mbalimbali nchini wameadhimisha miaka 52 ya Muungano kwa kufanya michezo na mazoezi
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO
-
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO
Siku 2 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni