SERIKALI INAJIPANGA KUFUNDISHA ATHARI ZA DAWA ZA KULEVYA TOKA SHULE ZA MSINGI ILI KUPUNGUZA TATIZO LA WATUMIAJI WA DAWA HIZO.

Serikali yajipanga kuanzisha klabu kwenye shule za msingi na sekondari kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi namna ya kutambua athari ya matumizi ya dawa za kulevya lengo likiwa ni kuokoa nguvu kazi ya taifa.

Licha ya umuhimu huo wa elimu,Jamii imetakiwa kuacha tabia ya kuwanyanyapaa vijana walioathirika na dawa za kulevya na badala yake wajitolee kuwasaidia kuwapeleka kwenye vituo vya afya ili wapate matibabu.
Mhandisi Stella Manyanya,Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi amesema serikali inatambua hatari waliyonayo vijana wanaotumia Dawa za kulevya na kupoteza nguvu kazi ya taifa.hivyo ni janga kubwa kwa taifa.
Frank John mkurugenzi wa soba kamba ya kweli inayowaunganisha vijana Pamoja na kituo cha kudhibiti dawa za kulevya ameiomba Serikali isaidie vituo hivyo ili kukomesha tatizo la uongezekaji wa watumiaji wa dawa za kulevya na kuachana na unyanyapaa.
Naye Kamishina wa polisi kandamaalum Mkoa wa dar es salaam Simon Nyakaro Sirro amesema Jeshi la polisi litaendelea kupambana na kudhibiti wafanyabiashara alamu wa dawa za kulevya kuingiza nchini na kuwataka vijana wote walioathirika wajiunge na vituo vya kulea waathirika wa dawa za kulevya ili kupata matibabu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List