Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Maambukizi ya Ukimwi, Dkt Fatma Mrisho amesema tatizo la Ukimwi bado ni kubwa kwa Vijana hali inayochangiwa na kufanya ngono zembe. Dkt Fatma amesema katika ukuaji wa tatizo hilo, Vijana wa Kike ndiyo wanaongoza kwa Maambukizi hayo ikilinganishwa na wale wa Kiume. hayo ameyasema wakati wa kufunga Semina ya Vijana kuhusu Ukimwi pamoja na Maambukizi ya VVU. James Kajingwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana nchini amewataka Vijana wajiepushe na Utumiaji wa Ulevi wa kupitiliza unaweza kuchochea tabia ya kufanya ngono zembe na kupelekea Maambukizi ya UVV, pia amewataka Vijana kujitambua sambamba kuwa Mabalozi wa wengine kwa ajili ya kulinda vizazi vijayo kwa kutoa elimu ya mapambano dhidi ya Maambukizi ya VVU
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO
-
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO
Saa 18 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni