MAGUFULI MWENYEKITI MPYA CCM ASHINDA KWA KISHINDO

Magufuli achaguliwa kwa kishindo
kuwa mwenyekiti mpya wa chama tawala nchini Tanzania(CCM).


Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama tawala nchini Tanzania CCM,kwa pamoja wamepiga kura ya ndiyo,kumuidhinisha rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuwa mwenyekiti watano wa chama hicho.Wajumbe walioshiriki kwenye mkutano mkuu na kupiga kura walikuwa ni 2398, ambapo mara baada ya zoezi la upigaji kura kuisha, mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mh Jakaya Kikwete, alimtangaza Rais Magufuli kamamshindi kwa kupata kura zote za ndiyo.

Awali kwenye kuelekea mkutano huu maalumu wa CCM,kulikuwa na taarifa za uwepo wa mgawanyiko ndani ya
chama, na taarifa kuwa mwenyekiti anayemaliza muda wake alikuwa hataki kuachia nafasi hiyo, tuhuma ambazo
zilikanushwa na Kikwete na Rais Magufuli.


Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi na kukabidhiwa rasmi vitendea kazi kama mwenyekiti wachama, Rais Magufuli, aliwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu, kwa kuendelea kumuunga mkono toka aliposhinda kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Rais Magufuli amesema kuwa, awali wakati rais Kikwete akimgusia kuhusu kumkabidhi nafasi ya uenyekiti wa chama,alikataa, hali iliyosababisha wazee wa chama kuingilia kati na
hatimaye kumshawishi kukubali.
Kwenye hotuba yake, Rais Magufuli amesisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano ndani ya chama, kama nguzo muhimu ya kufikia malengo na utekelezaji wa ilani ya chama.
Mwenyekiti huyo mpya, ameapa kupambana na ufisadi kama njia ya kuhakikisha anakomesha vitendo vya rushwa ndani ya chama na kwenye taifa kwa ujumla.Miongoni mwa masuala ambayo Rais Magufulu amesema
ataanza nayo pindi atakapoanza kazi ni pamoja na :Utendaji kazi wa chama, mfumo wa uongozi, kuondoa na
kupunguza baadhi ya vyeo ambavyo havina msingi ndani ya chama, maslahi ya wafanyakazi wa chama tawala,kupitia na kuhakiki mali za chama, umoja na mshikamano, mapambano dhidi ya Rushwa pamoja na kuhakikisha chama kinaongeza idadi kubwa ya wanachama.
Rais Magufuli amesema pia,atahakikisha anawaondoa wasaliti wa ndani ya chama na kwamba katika utawala wake
hatakubali kuwa na wanachama ambao ni wasaliti.
Magufuli ameongeza kuwa wakati wa uongozi wake,atahakikisha chama kinajitegemea kwa rasilimali badala ya
kuwa omba omba kwa wafadhili ili kiendeshe shughuli zake.Utekelezaji wa asilimia mia moja wa ilani ya chama chake, ni miongoni mwa masuala ambayo Rais Magufuli amesema
atahakikisha anafanikisha.


Magufuli anakuwa mwenyekiti wa tano wa chama tawala nchini Tanzania, baada ya watangulizi wake, aliyekuwa
muasisi wa chama hicho, marehemu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete ambao wote hawa walikuwa marais wa Tanzania kwa nyakati tofauti.

Wadau wengi na Makada wameonyesha kufurahishwa na hali hiyo Kutokana na Ukweli kwamba Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ni mtu ambaye anachukia rushwa sana akiongea na Mwandishi wa Mtandao huu Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Mbagala kura za maoni Ccm ndugu Stuart George Matola amesema huo ni ushindi wa dememokrasia ambao unatokana na Ccm tu na hakuna Chama kingine cha Siasa kinaweza kufanya hivyo bila ya kuathiri umoja wao.Akimuongelea Mwenyekiti mpya amesema Ana uhakika naye ni mtu wa mabadiliko ya kweli na Mahakama MUNGU hivyo Wana CCM tunategemea mazuri toka kwake. 

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List