Naibu Waziri wa Elimu afanya ziara shule ya Watoto wenye Ulemavu Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko kwa ajili kujua maendeleo yao, hali ya Madarasa, vitendea kazi pamoja na Mazingira ya Walimu katika ufundishaji. Mhandisi Stella Manyanya katika Ziara yake hiyo amebaini changamoto za upungufu wa Vifaa vya kufundishia watoto hao wenye Ulemavu wa Viungo sambamba na ukosefu wa karatasi, vitabu na Walimu kwa watoto Wasioona na kusikia.Naye Mwalimu Mkuu wa Uhuru Mchanganyiko Anna Mshana amefurahishwa sana na Ujio na kusema kuwa yeye pamoja na Walimu wote wamefarijika kuona Serikali inatekeleza ahadi zake kwa vitendo na kuwafikia walengwa wake.Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya alizingumzia bajeti ya Serikali kwa Wizara yake na kusema tayari fungu kubwa limeandaliwa kwa ajili ya kuelekezwa kwa Wanafunzi wenye Ulemavu nchini na kuwatia Moyo wanafunzi hao kusoma Masomo ya Sayansi ili kuweza kuisaidia Serikali katika suala la ajira hususani uwezo wa kujiajili.
KING KIKII KUAGWA LEADERS CLUB
-
Le Maestro Kikumbi Mwanza Mpango (King Kiki) pichani enzi za uhai wake .
*TANZIA*
Mwanamuziki nguli mwenye asili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo...
Saa 9 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni