Mfanyabiashara wa Nafaka katika maeneo ya Vingunguti Jijini Dar es salaam Salatiel Chengula ameiomba Serikali kuzingatia kwa ukaribu benki binafsi Kwa madai zimekuwa zikionyesha kiuka sheria na taratibu za nchi na kusababisha usumbufu kwa wateja.
Chengula Akiwa ni miongoni mwa wahanga wa ukikwaji wa sheria hizo, amedai kuwa Acces benk imeng'ang'ania Hati zake mbili za nyumba licha ya kukamilisha taratibu za kurejesha mkopo wake miaka sita iliyopita.
Mwandishi wa Mtandao huu alienda Makao Makuu ya Acces Benk kuulinzia suala hilo, na kukutana na Mwanasheria wa Benk hiyo hata hivyo alikataa kutowa ushirikiano kwa wandishi habari..
Mwandishi alienda mbali zaidi Wizara husika na kuambiwa Benk kuu kuna dawati linalohusika na Migogoro ya Kibenk. Ganga Mlipano Meneja Msaidizi Dawati la kutatua Migogoro ya Wateja wa Kibenki ambapo amesema Serikali imeamua kuanzisha dawati hilo baada ya kubaini Wateja wengi wamekuwa wakipata usumbufu wa kurudishiwa Hati zao baada ya kukamilisha mrejesho wa mkopo. ametowa wito kwa wananchi wenye Shida au migogoro na mabenki kufika katika dawati hilo kwa ajili ya kutatuliwa Shida hizo na kupata ufumbuzi wa Migogoro yao na mpaka sasa tayari dawati limeshatatua malalamiko ya watu 112 kwa muda ya mwaka mmoja tangu kuanza kwa dawati hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni