WANANCHI WAMEMUOMBA RAIS JOHN Pombe Magufuli awasaidie suala la Tazara Kutowa Notice ya miezi miwili makazi ya Wananchi

Siku chache tangu Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia TAZARA kutoa notisi ya miezi miwili ya kuwataka Wananchi wote walio jenga kando kando ya Reli kubomoa Majengo yao na kuyaacha wazi kwa madai kuwa wavamizi. Wananchi awakubaliani na Mamlaka hiyo kwa kuwaita Wavamizi.  Wananchi wamedai Mamlaka hiyo haijawatendea haki kuwataka waondoke kwenye maeneo hayo bila kulipwa fidia zao Kwakuwa wameishi zaidi ya miaka 20 na wengine zaidi miaka30 tangu kuanzishwa kwa Reri hiyo wakati wa Hayati Mwalimu Julias Kambarage Nyerere akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwataka Wananchi wawe Walinzi wa Miundombinu ya Reli kwakuwa ni mali yao Wananchi. Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdallah Mtolea akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu Ameitaka Mamlaka hiyo kuwaonyesha Sheria za TAZARA za mwaka 1975 na Sheria ya Mwaka1995 inayoonyesha uhalali wa Mita za ukubwa wa maeneo ya Reli uhalali wa Mamlaka hiyo kuwaondoa katika maeneo hayo. Aidha  Mbunge huyo ameitaka TAZARA kuwalipa fidia wananchi wake endapo wanadhamiria kuwaondoa.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List