Mahakama ya katiba yamtangaza Ali Bongo rais wa Gabon

Rais Ali Bongo wa Gabon

Rais Ali Bongo wa Gabon
Mahakama ya katiba nchini Gabon imethibitisha kuwa Ali Bongo ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 27 nchini humo.
Rais Bongo amepata 50,66% na mpinzani wake, mwenyekiti wa zamani wa Muungano wa Afrika Jean Ping 47,24%.
Matokeo ya awali yalionyesha ushindi wa Bongo kwa tofauti ndogo ya kura takriban 6000.
Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho rasmi yaliotolewa na mahakama ya katiba Bongo alishinda na kura zaidi kutokana na kutobatilisha kura zilizopigwa katika ngome ya kiongozi huyo Haut-Ogoue.
Hatahivyo kura katika vitu 21 mjini Libreville zimefutiliwa mbali kutokana na ombi la upande wa kampeni ya rais. Na ndio sababu kiongozi huyo amepata asilimia kubwa zaidi katika matokeo ya mwisho.
 Mpinzani nchini Gabon, na aliyekuwa mwenyekiti wa Muungano wa Afrika Jean Ping
Mpinzani nchini Gabon, na aliyekuwa mwenyekiti wa Muungano wa Afrika Jean Ping
Upinzani uliwasilisha malalamiko kupinga matokeo ya awali ya uchaguzi na kuiomba mahakama iamrishe kuhesabiwa upya kura hizo, katika eneo hilo la Haut-Ogoue, magharibi mwa Gabon ambapo rais Bongo ana wafuasi wengi.
Kumekuwa na wasiwasi katika mji mkuu Libreville kwamba huenda ghasia zikazuka baada ya mahakama ya katiba kutoa uamuzi wake.
Baadhi ya wakaazi walionekana kununua vyakula na kuweka akiba nyumbani.
Raia mmoja ameiambia BBC: " Nadhani kuna wasiwasi, watu wanataka kuwa salama, wanataka kununua vitu na kusubiria matokeo kwa makini nyumbani, iwao kila kitu kitakwenda sawa itakuwa vizuri"
Maduka mengi yameamua kufunga biashara kukwepa uporaji.
Mapema mwezi huu biashra nyingi ziliathirika.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List