16.22pm:Na mechi inakamilika hapa Manchester United ikiibuka kidedea baada ya kuicharaza Leicester City 4-1
16.17pm: Dakika za lala salama Manchester United bado iko kifua mbele hapa dhidi ya Leicester City.
16.14pm: Mata anatoka Ashley Young anaingia16.11pm: Na Rooney sasa anaingia kwa upande wa Manchester United
16.10pm: Dakika ya 82 Manchester United 4-1 Leicester City
16.09pm: Namuona Wayne Rooney akivaa jezi ishara kwamba huenda akaingia wakati wowote kutoka sasa
16.08pm: Carrick anaingia kwa upande wa Manchester United.
16.06pm: Leicester wanajaribu kila mbinu hapa kusawazisha lakini hali si hali kipa David De Gea anapangua mkwaju mwengine wa mfungaji wa bao la kwanza wa Leicester Gray
15.55pm: Leicester wanaamka hapa baada ya Kujipatia bao la kwanza ,na sasa wachezaji wa Man United wanalazimika kurudi nyuma ili kulinda lango lao
15.47pm: Gooooooooooal Leicester wapata bao lao la kwanza hapa kupitia mchezaji Gray baada ya kuwachenga viungo wa kati wa Man United na kupiga mkwaju ambao david De Gea hakuona kitu.
15.46pm: Leicester wamenyamazishwa hapa,na United inaendelea kutawala mechi
Kipindi cha pili kinaanza hapa kwa kasi huku Man United wakitaka kuongeza bao la tano dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi Leicester
Na kipindi cha kwanza kinakamilika hapa Vijana wa Man United wakiwa kifua mbele.
15.12pm: Manchester United 4-0 Leicester
15.11pm: Goooooooooooal Pogba hatimaye aitikisia wavu timu yake hapa kwa mara ya kwanza baada ya kukosolewa kwa mda mrefu
15.09pm: Goaaaaaaaaaaal Manchester United wanajipatia bao ya tatu kupitia kijana Rashford hapa .Wachezaji wa Leicester wanalaumiana hapa
15.07pm: Manchester United 2-0 Leicester City
15.06pm: Gooooooooooooal ...Pogba aonana na mata vizuri hapa katika lango la Leicester kabla ya Mata kufunga bao la pili kwa niaba ya manchester United
15.02pm: Kwa kweli hawa wachezaji wa Leicester wanacheza kana kwamba tayari wamesalimu amri.kwani wamerudi nyuma na wanawacha wachezaji wa Man United kuwavamia kiholela
15.00pm: Manchester United sasa wanachukua udhibiti wa mechi hii na kusababisha hatari baada ya hatari katika lango la Leicester.
14.56pm: Manchester wanalivamia tena lango la Leicester ,Pogba achukua mpira na kumpatia pasi nzuri Ibrahimovic ,lakini anapiga mpira nje akiwa amebakia na goli.
14.55pm: Manchester United wavamia lango la Leicester hapa ,Ibrahimovic ampatia pasi muruwa Rashford ambaye alikuwa amebakia na kipa lakini anaupiga mpira unakuwa mwingi na unatoka lo.Rashford anakosa bao la wazi hap.
14.53pm: Manchester United 1-0 Leicester
14.52pm: Goooooooooooal Manchester United wanaongoza hapa baada ya Chris Smalling kufunga kona iliopigwa na Daley Blind.
14.51pm: Wanapanga mpira vizuri hawa wachezaji wa manchester United mbele ya lango la Leicester ,lakini wenye lango wanakataa.
14.49pm: Leicecter sasa wanaamka na kuanza kudhibiti mpira
14.46pm: Hatari pale katika lango la Man United baada ya kona kupigwa huku mabeki wa Mourinho wakilazimika kufanya kazi ya ziada kuwazuia washambuliaji wa Leicester.
14.45pm: Manchester United wanafanya masihara hapa na mpira unnatoka kona
14.42pm: Kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza Leicester City
14.40pm:Kikosi cha Manchester United
14.39pm: Pogba anatafuta mipira ya kumlisha Ibrahimovic lakini mabeki wa Leicester wako chonjo sana.
14.38pm: Mechi inaanza kwa mbwembwe hapa huku Manchester United ilio na wachezaji wa bei ya juu wakijaribu kuipita ngome ya Leicester
14.30pm: Manchester United vs Leicester City imeanza
Huku
mabingwa wa zamani wa ligi ya Uingereza Manchester United wakikabiliana
na mabingwa wa ligi msimu uliopita Leicester City, mkufunzi wa
Manchester United Jose Maourinho anasema kuwa Wayne Rooney ameathiriwa
na ukosoaji aliopata baada ya ushindi wa timu ya Uingereza dhidi ya
Slovakia.
0 comments:
Chapisha Maoni