SERIKALI YA AWAMU YA TANO IMESHINDWA KUFANYA VIZURI SEKTA MUHIMU.

Tangu Rais Mpya wa Tanzania kuchaguliwa Dkt John Pombe Magufuli umeisha mwaka bila kuonekana hata dalili ya maendeleo katika sekta muhimu zote nchini.
Wakitoa maoni wananchi na wadau mbalimbali wamelalamikia kuwa serikali ya Awamu ya Tano kushindwa Kabisa kufanya mambo waliyo ahidi na badala yake kufanya mambo ambayo sio vipaumbele vilivyowaweka madarakani.
Katika serikali ya Awamu ya Tano Elimu inazidi kuonekana kushuka zaidi licha ya juhudi za kuongeza madawati Tu kupewa nguvu lakini uhaba wa walimu umekuwa changamoto kubwa huku Serikali ikishindwa Kabisa kuajiri walimu wapya.Pia vifaa vya kufundishia na kufuta baadhi ya posho za walimu kumefanya sekta hiyo kukosa muelekeo na kupunguza ufanisi wa watumishi wa Sekta hiyo.Waziri wa elimu amekua tatizo kubwa kutokana na Maamuzi ya kukurupuka bila kuangalia athari za maamuzi au taarifa zake anazotoa kwa vyombo vya habari.Kukosekana kwa malengo ya Elimu pia,kwa serikali ya Awamu ya tano kumefanya sekta ya Elimu kuwa na uwezo mdogo wa kufanya vijana wanaohitimu kuweza kuisaidia nchi.

Suala la Ajira pia limekuwa changamoto na tatizo kubwa ukizingatia hii ilikuwa ahadi ya Mh.Rais kipindi cha uchaguzi kuwa ataajiri mapema zaidi mwaka 2016 lakini mpaka sasa hakuna dalili ya ajira za walimu na watumishi wa afya.Mikopo kwa wanafunzi imezidi kuwa kitendawili kuliko serikali zote zilizopita.Tanzania ya Viwanda bado ni Jipu kutokana na ukweli kuwa hakuna dalili yoyote ya Tanzania hiyo huku viwanda ambavyo Tayari vimeota mizizi kufungwa na vingine kuachisha Kazi zaidi ya watanzania 30000(elfu thelathini)

Hata hivyo Serikali imejikita kufanya mambo ambayo hawakuwahi kuhaidi katika uchaguzi kama vipaumbele kama Ununuaji wa ndege,kuhamisha serikali dodoma na ujenzi wa mabweni na miundombinu ambayo haipo katika bajeti licha ya kuwa vitasaidia Tanzania lakini si vipaumbele kwa wakati huu.Na kumaliza fedha za serikali huku hali ikizidi kuwa Ngumu kwa Mwananchi wa kipato cha chini.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List