ZIARA YA TANESCO

Shirika LA umeme nchini Tanesco limeilalamikia Halmashauri ya jiji LA Dar es salaam kwa kutotoa ushirikiano na shirika hilo wakati wa kupitisha miundombinu Sanjari na upimaji wa mipango miji.
Aidha shirika hilo limewekeza zaidi ya shilingi trillion 5.3 kwa ajili ya ujengaji wa mitambo ya kisasa na ukarabati ambapo Dar es salaam wamejenga vituo 32 vya ugawaji umeme.
Kwa kuzingatia kasi ya ukuaji wa uchumi baadhi ya maeneo kwa kuzingatia umuhimu wa eneo,Tanesco imefungua kituo kipya Kabisa cha kisasa hospitali ya muhimbili ili kukomesha kabisa tatizo la umeme hospitalini hapo.
Pia imekiongezea nguvu kituo cha usambazaji umeme cha katikati ya mji(New city center) kwa kupokea umeme wa kilowatts 132 na kugawa killowatts 33 kwa vituo vidogo.
Lengo la kuleta umeme wa kisasa ni katika kufikia Tanzania ya viwanda.
Licha ya mradi mkubwa uliohusisha vituo takribani 29 vya jiji la dar es salaam,Mradi huo Mkubwa wa umeme Kutoka Iranga mapaka shinyanga(BACKBONE)ndiyo unasemekana kuwa mradi mkubwa zaidi kuwahi kutokea Tanzania tangu tunapata Uhuru na wa pili kusini mwa janga la Sahara nyuma ya afrika kusini.

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List