UFUGAJI WA SAMAKI.

Wahitimu wa mafunzo ya ufugaji samaki wa CHUO cha Mbegani,Wilaya ya Bagamoyo MKOA wa Pwani wametakiwa kutumia fursa waliyoipata na kuwa wajasiriamali Waziri ili waweze kujiajiri na kuwaajiri vijana pakoja na kuwa mabalozi kwa kutoa elimu ya kupiga vita uvuvi haramu.
Hayo yamesemwa na mkuu wa WILAYA ya Bagamoyo,Mh:Majid Hemed Mwanga wakati mahafali ya wanachuo 21wa wilaya ya Bagamoyo waliokuwa chini ya VETA kwa ufadhili wa benki ya Maendeleo Africa.
Mkurugenzi wa CHUO cha uvuvi Mbegani,Yahya Mgawe amesema uharibifu wa rasilimali za Bahari unatokana na wavuvi kukosa mbinu Za uvuvi pamoja na uhitaji wa samaki soko la kimataifa kuongezeka.
Kaimu Mkurugenzi wa Beta kanda ya Mashariki.Asanterabi Kanza ameishukuru Banki ya Afrika ya Maendeleo kwa kutoa mchango huo kuwawezesha wananchi wa Bagamoyo kupata mafunzo na kuwataka wahitimu hao kuitumia vyema elimu waliyopata kwa maendeleo katika sekta ya uvuvi bagamoyo.
Serikali kwa sasa inasisitiza wananchi wake kufanya ufugaji wa samaki kwa njia ya mabwawa  ili kutunza mazingira na kujiongezea kipato.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List