Watoto waongezeka wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Ongezeko kubwa la makundi hatarishi kwa watoto waishio katika kata ya keko wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam,limedaiwa kuchangiwa na wazazi wengi kuzaa kiholela huku maisha yao yakiwa duni kiuchumi na kushindwa kuwamudu katika kuwapatia mahitaji.
Diwani wa kata ya Miburani Juma Mkenga katika mkutano wa hadhara wa watoto ulioandaliwa na wadau wa haki za binadamu katika mitaa ya keko machungwa amesema tatizo LA watoto wengi kushindwa kusoma shule linachangiwa na wazazi kutokana na kuzaa watoto wengi wanaojiingiza katika tabia mbaya kama za ushoga,uhalifu,na kutumia dawa za kulevya au hata kujiuuza.
Ameongeza pia katika Kata yake kuna ongezeko kubwa la watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kutokana na wazazi kukwepa majukumu ya ulezi wa watoto hao.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Mkutano wa Haki za watoto kata ya Miburani,Emijidius Cornel amesema,kumekuwepo na tatizo kubwa katika kata hiyo,la watoto kupata elimu bora na kuiomba Serikali ibadili mtaala utakaowezesha somo la kiingereza kufundishwa kuanzia ngazi ya msingi.
Baadhi ya wadau na wananchi wamesema Serikali ya  awamu ya tano inatakiwa kufanya marekebisho ya mfumo wa elimu na mitaala yake kwa ujumla.

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List