Baraza la kuu la Uongozi la Chama cha wananchi CUF limeiagiza kamati ya maadili na nidhamu kumuhoji katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad kwa madai ya kuhusika na njama ya kukihujumu chama hicho.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama cha CUF Profesa Lipumba katika juhudi zake za kuimarisha chama cha CUF ambapo karibuni kimeonekana kuyumba na kutawaliwa na migogoro. Profesa Lipumba amesema katiba na sheria zilizounda bodi ya wadahamini CUF na halali hivyo kupingana na juhudi hizo ni hujuma dhidi ya Chama cha CUF.
Pia amesema Maalim Seif Sharif Hamad hana uwezo wa kupinga au kufungua kesi dhidi ya bodi ya wadahamini ya Chama cha wananchi CUF.
Mapema chama cha CUF kilichagua bodi ya wadahamini kupitia baraza kuu la Chama hicho na kupishwa na kusajiliwa rasmi. Lakini bodi hiyo ilipingwa vikali na Katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad kwa madai inataka kumtoa kwenye nafasi yake na kuwakosesha haki Wana CUF.
DKT. DORIYE AVISHWA CHEO KUAPISHWA KUWA KAMISHNA WA UHIFADHI NCAA.
-
*Na Kassim Nyaki, Karatu.*
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb) kwa niaba
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Sa...
Siku 4 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni