Mheshimiwa Diwani NURU AWADHI wa viti maalamu wa Wilaya ya Ilala ambaye anawakilisha kundi la watu wenye ulemavu ametoa msaada kwa kwa watoto wenye ulemavu na wazima kwa ajili ya kujifunza elimu ya dini ya Kiislamu. Mheshimiwa Diwani Nuru ametoa msaada vitabu dini ya Kiislamu na Mashine kwa ajili kuandika na kujifunza kwa watu wenye ulemavu wa macho.
Mheshimiwa Diwani Nuru Awadhi alifuatana na Mwenyekiti wa Buguruni ambaye kwa pamoja wamesema serikali imetenga bajeti kwa ajili ya makundi maalum lakini juhudi za viongozi ni chachu za kufanikisha malengo ya kugusa hayo makundi maalum na kutolea mfano kwa Diwani wa viti maalamu Nuru jinsi alivyopigana kupata vifaa hivyo.
Kwa niaba ya wanafunzi wa wanufaikaji wa msaada huo aliongea kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Diwani Nuru Awadhi ambaye alisema pia aliwahi kuwa mwanafunzi wake kipindi cha chuma.
Vifaa hivyo alivyotoa Diwani Nuru baadhi alitoa ela zake mwenyewe na baadhi kuomba msaada kwa marafiki zake waishiyo afrika kusini. ukiwepo na ubao wa kufundishia, Vitabu na Mwisho amewataka walimu na wanafunzi kutumia msaada waliopata wa vifaa hivyo vizuri ili waweze kuwa mabolozi wazuri baadaye.
0 comments:
Chapisha Maoni